Sura za hivi majuzi za Biblia

Zaburi 150

1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. 2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. 3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; 4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; 5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.

Soma

Zaburi 149

1 Haleluya. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa. 2 Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao. 3 Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie. 4 Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu. 5 Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao. 6 Sifa kuu za Mungu na ziwe…

Soma

Zaburi 148

1 Haleluya. Msifuni Bwana kutoka mbinguni; Msifuni katika mahali palipo juu. 2 Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni, majeshi yake yote. 3 Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga. 4 Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu. 5 Na vilisifu jina la Bwana, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa. 6 Amevithibitisha hata milele na milele, Ametoa amri wala haitapita. 7 Msifuni…

Soma